ALICHOKISEMA DIAMOND JUU YA KUHUSISHWA NA FREEMASON!!

Monday, June 11, 20120 comments

Ili kumaliza utata wa je, Diamond ni Freemason au la, Ijumaa Wikienda lilibeba jukumu la kumtafuta ili aanike ukweli wake ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Unajua mwanzoni nilikuwa sikumbuki ni lini na wapi nilipiga picha ya dizaini hiyo. ‘Anyway’, isiwe kesi, nakumbuka ilikuwa Uingereza kipindi kile nilikuwa na shoo nchini humo.
“Nakumbuka walinifuata watasha wengi
tofauti lakini huyo mmoja alining’ang’ania sana nipige naye picha.

“Kwa kweli alinilazimisha sana kwa sababu mwanzo nilikataa lakini baadaye nikaona isiwe ishu nikampa ushirikiano alioutaka.
“Mimi sikuona matatizo alivyotaka tusalimiane kwa kugusisha vidole kwa sababu nilikuwa sijui chochote kuhusu Freemason. Nimeijua baada ya mambo haya kuyasikia kwa sana hivi karibuni.
“Kwa hiyo inawezekana siku hiyo waliniunganisha bila mimi kujua (kicheko).” Habari kutoka Ijumaa Wikenda.
Share this article :

TUPE MAONI YAKO HAPA!!!!

KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU HAPO CHINI BOFYA ''LIKE''

.

.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. THE FRESH 2015 - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger